Alhamisi, 17 Aprili 2014
Categorized |
MAJIRANI WAMLALAMIKIA JIDE KWA UCHAFU
08:06
MAJIRANI wanaoishi karibu na mwanamuziki wa kizazi kipya Bongo,
Judith Wambura ‘Jide’ wamelalamika kwamba mwanamuziki huyo ameiweka
nyumba yake katika mazingira ya uchafu yanayohatarisha maisha yao.
Wakizungumza na Amani, majirani hao wanaoishi Kimara-Temboni jijini
Dar, walisema mwanadada huyo ameacha vichaka vikubwa vinavyoizunguka
nyumba yake hali ambayo ni hatari kwani nyoka wanaweza kufanya makazi
hivyo kusababisha maafa kwa watoto na watu wazima.
“Yaani huyu mwanamuziki Jaydee ametuachia kichaka, yeye na mumewe hawataki kufanya usafi kuizunguka nyumba yao hali ambayo inatupa wasiwasi sisi majirani, tuna watoto wanaweza kung’atwa na nyoka kwani nyoka hupenda kuzaliana kwenye vichaka kama hivi,”
alisema jirani mmoja ambaye hakutaka kutajwa jina lake gazetini.
Waliendelea kusema kuwa, Jide hana hausigeli wala ndugu yeyote anayeishi naye, inawezekana ndiyo maana anashindwa kufanya usafi kuzunguka nyumba yake.
“Lady Jaydee anaishi na mumewe (Gardner) tu labda ndiyo sababu ya kushindwa kutunza mazingira, majani yameota mpaka kero. Tumeshapeleka malalamiko yetu serikali ya mtaa lakini hajaitwa kuambiwa, tunashangaa,” alisema jirani huyo.
Baada ya kuzinyaka habari hizo, gazeti hili lilimtafuta Jide na mumewe Gardner ambapo mume huyo ndiye aliyepatikana na kusomewa madai hayo. Baada ya kusikiliza mpaka mwisho, Gardner alijibu:
“Kama wamesema hivyo mimi sina la kujibu (no comment)”.
Juzi, mapaparazi walifika kwenye ofisi ya serikali ya mtaa lakini ilikuwa imefungwa
CHANZO;HABARI KWANZA
This post was written by:
BTDesigner - who has written 18 posts on The Gazette Edition Blogger.
In this space you can include a little "About the Author" section to inform your readers about the author's background and specific niches. It doesn't have to be long, but it doesn't need to be short either. Nice little feature to Gazette this, isn't it?
Jisajili kwenye:
Chapisha Maoni (Atom)
0 Responses to “MAJIRANI WAMLALAMIKIA JIDE KWA UCHAFU ”
Chapisha Maoni